#Football #Sports

KWA KUMBUKUMBU ZA CARLES MINARRO

Kocha wa Barcelona Hansi Flick amesema timu yake itamenyana na Benfica kwenye Ligi ya Mabingwa
siku ya Jumanne ikiwa ni mchezo wa kumbukumbu kwa daktari wa klabu Carles Minarro, aliyefariki
Jumamosi.

Miamba hao wa Catalonia wanaongoza kwa bao 1-0 katika mechi ya 16 bora kutoka kwa mkondo wa
kwanza mjini Lisbon kabla ya pambano hilo kwenye Uwanja wa Olympic.

Mechi ya Barcelona ya La Liga Jumamosi dhidi ya Osasuna iliahirishwa dakika 20 kabla ya kuanza baada
ya daktari huyo mwenye umri wa miaka 53 kufariki alasiri hiyo.

Daktari Minarro amekuwa akifanya kazi na timu tofauti za Barcelona tangu 2017, na alianza kufanya kazi
na timu ya kwanza ya kandanda ya wanaume miezi michache iliyopita.

Barcelona iliifunga Benfica 5-4 mjini Lisbon katika hatua ya makundi na kisha tena ikiwa na wachezaji 10
kwa muda mwingi wa mchezo wiki iliyopita baada ya Pau Cubarsi kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Hata hivyo Flick alisema kikosi chake hakitasonga mbele katika hatua ya robo fainali kama ilivyopangwa,
huku Benfica wakiichapa Juventus ugenini katika hatua ya makundi na kuitoa Atletico Madrid nyumbani.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KWA KUMBUKUMBU ZA CARLES MINARRO

CHANGAMOTO ZA MDHIBITI WA BAJETI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *