RUTO AKOSOA MFUMO WA UN, AU

Rais William Ruto amekariri kujitolea kwa serikali yake katika kurejesha utulivu nchini Haiti, akiahidi kuwatuma polisi zaidi nchini humo ili kufikisha jumla ya polisi 2,500 kufikia Januari mwaka ujao.
Akizungumza katika kongamano la umoja wa mataifa UN nchini Marekani, Ruto ametetea hatua hiyo na kuwapongeza polisi wa Kenya kutokana na umahiri wao wa kukabili magenge ambayo yameteka baadhi ya maeneo muhimu ya Haiti.
Wakati uo huo, Ruto amelishutumu baraza la usalama la umoja wa mataifa, kwa madai ya kushindwa kutekeleza majukumu yake.
Aidha, Ruto amependekeza mageuzi katika baraza hilo, saw ana katika muungano wa umoja wa Afrika AU.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa