WIZARA YA VIJANA YAZINDUA KAMATI YA JINSIA NA UTEKELEZAJI LEO
Wizara ya masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo inapanga kuzindua kamati ya masuala ya jinsia na utekelezaji hii leo.
Hafla hiyo itaongozwa na waziri wa masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo Kipchumba Murkomen, na inapangiwa kuandaliwa katika jumba la Talanta Hela muda wowote kuanzia sasa.
Kamati hiyo imejukumiwa kuimarisha usawa wa kijinsia na kulinda haki za kila mmoja anayehusika katika sekta za vijana, michezo na ubunifu.
Lengo lake ni kutoa mwongozo wa kisera wa kuimarisha mazingira jumuishi na salama kwa washirika wote wa sekta hizo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































