MAANDAMANO YALEMAZA BIASHARA BOMET

Barabara kuu ya Kisii kuelekea Narok imefungwa kwa zaidi ya saa tatu na waandamanaji mjini Bomet ambao wanaandamana kulalamikia uongozi duni kwenye kaunti hiyo.
Wakati wa maandamanao ya leo, vurugu zimeshuhudiwa baada ya makunndi mawili kukabiliana kwa mawe na kusababisha wafanyabiashara wengi kufunga biashara zao.
Hata hivyo, waandamanaji wamemlaumu gavana Hillary Barchok kutokana na vurugu hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa