MCF FC YAIBWAGA MOMBASA UNITED 3-0 KATIKA MECHI YA NSL

MCF FC iliifunga Mombasa United mabao 3-0 katika mechi ya Ligi ya Kitaifa Daraja la Pili (NSL) kwenye Uwanja wa Serani, Mombasa. Mabao ya MCF yalifungwa na James Olweny, John Okoth, na John Ochieng.
Olweny alifunga bao la kwanza dakika ya 30 baada ya pasi safi kutoka kwa Ezekiel Okare. Okoth aliongeza la pili dakika 10 baada ya kipindi cha pili kuanza, na Ochieng alikamilisha ushindi dakika ya 72 baada ya ushirikiano mzuri na Okare.
Mombasa United walijaribu kurejea kwa kuwaingiza wachezaji wenye uzoefu, lakini walishindwa kupenya ngome ya MCF. Mshambuliaji Jackson Maruga karibu afunge bao la kufuta machozi, lakini kipa wa MCF, Otieno Were, alizuia.
Kocha wa Mombasa United, Amadi Said, alionyesha kutoridhika, huku kocha wa MCF, Vincent Nyaberi, akipongeza timu yake kwa ushindi huo mkubwa.
Imetayarishwa na Janice Marete