#Sports

SEVILLA WAPATA KOCHA MPYA

Sevilla mnamo Jumatatu ilitangaza uteuzi wa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Argentina Matias Almeyda kama kocha mpya wa klabu hiyo ya Uhispania kwa mkataba wa miaka mitatu.

Almeyda mwenye umri wa miaka 51 anajiunga na Sevilla baada ya misimu mitatu na AEK Athens ya Ugiriki, ambapo alishinda ligi na vikombe mara mbili mnamo 2022-23.

Pia aliwahi kutamba katika Ligi Kuu ya Soka akiwa na San Jose Earthquakes baada ya kufundisha River Plate na Banfield katika nchi yake, pamoja na klabu ya Mexico ya Guadalajara.

Almeyda anarejea katika klabu aliyoiwakilisha kama mchezaji karibu miongo mitatu iliyopita. Aliichezea Sevilla mnamo 1996-97 kabla ya kucheza Lazio, Parma, Inter Milan na Brescia za Italia.

Kiungo huyo wa zamani aliichezea Argentina mechi 40.

Almeyda anachukua nafasi ya Joaquin Caparros, aliyeletwa kwa kipindi kifupi cha nne Sevilla mwezi Aprili baada ya kutimuliwa kwa Francisco Garcia Pimienta.

Sevilla walimaliza katika nafasi ya 17 kwenye La Liga na pointi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja.

Imetayrishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *