#Local News

RIPOTI YA KIFO CHA OGOLA KUWEKWA WAZI KWA UMMA

Ripoti ya kifo cha aliyekuwa mkuu wa majeshi nchini Francis Ogola itawekwa wazi kwa umma.

Kwa mujibu wa Waziri wa ulinzi Aden Duale uchunguzi unaendelea na kwamba maafisa kadhaa wanaochunguza ajali hiyo waliyachukua mabaki ya ndege hiyo ya kijeshi na kuyapeleka nchini marekani hasa katika kampuni ya Bell Textron Inc iliyounda ndege hiyo katika juhudi za kufanikisha uchunguzi.

Duale vile vile amesema kwamba sampuli za mabaki hayo na za vipimo kadhaa vya eneo la ajali vilichukuliwa na maafisa wa jeshi zikiamilika kwamba zitasaidia pakubwa klatika uchunguzi.

Duale aidha amepuuza madai kwamba vifaa vingi vya kijeshi nchini vimekuwa vya zamani na kwamba ndio sababu ya ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Ogola na maafisa wenzake wa kijeshi katika kauli ambayo huenda ikaibua maswali mengi , duale anasema kwamba ndege iliyomuua rais wa Iran Ibrahimu Raisin a watu wengine 6 ilikuwa ya kampuni moja na ile iliyokuwa imembeba marehemu OgolaOgola na maafisa wengine 9 wa ngazi ya juu katika idara ya jeshi walioaga dunia mwezi uliopita wa aprili kufuatia ajali ya ndege iliyotokea katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet.

Imatayarishwa na Janice Marete

RIPOTI YA KIFO CHA OGOLA KUWEKWA WAZI KWA UMMA

GAVANA KAHIGA, SUDI WAMJIBU MALALA

RIPOTI YA KIFO CHA OGOLA KUWEKWA WAZI KWA UMMA

RUTO AONGOZA HAFLA YA MAOMBI YA KITAIFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *