WATANO WAFARIKI KWENYE MGODI RONGO
Watu 5 wamefariki baada ya ukuta wa mgodi kuporomoka na kuwaangukia walipokuwa wakichimba migodi katika eneo la Rongo kaunti ya Migori.
Akithibitisha kisa hicho, Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo George Matundura, amesema watu zaidi wangali wamekwama kweny mgodi huo na kuongeza kwamba juhudi za uokozi zinaendelea.
Aidha, ameahidi kwamba serikali itaweka mikakati ya kuimarisha usalama wa shughuli za uchimbaji migodi eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































