MALIKI WATAMBA BUNGOMA
Shule Ya Upili Ya Wavulana Ya Maliki Ndio Washindi Wa Mwaka Huu Wa Mashindano ya Shule Za Upili Kwa Upande Wa Kandanda Kaunti Ndogo Ya Bungoma Kaskazini Kwa Kuicharaza Shule Ya Upili Ya St.Patricks Naitiri Bao Moja Bila Jawabu.
Kwenye Semi Fainali Ya Kwanza Shule Ya Upili Ya Maliki ilichapa Sirakaru Bao Moja Kwa Bila.
Semi Fainali Ya Pili Shule Upili Ya Wavulana Ya St.Patricks Naitiri iliishinda Nabing’eng’e Kwa Mabao Mawili Kwa Moja .
Fainali Kwa Upande Wa Wasichana Mbakalo Waliibuka Washindi Moja Bila dhidi ya Bwami.
Hayo yakijiri kwenye voliboli ya Wavulana , Shule Ya Upili Ya Kibisi Kibisi Waliibuka Washindi Dhidi Ya Maliki Kwa Seti Tatu Kwa Sufuri.
Kwa Upande Wa Voliboli Wasichana Kibisi Ilishinda Bilibili Set Tatu Kwa Moja.
Netiboli Kibisi Walishinda Eluuya Kwa Mabao 21kwa 14 Na Kuibuka Washindi Mwaka Huu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































