FORD KENYA YAKANA KUVUNJWA

Chama cha Ford Kenya kimepinga madai ya kuvunjiliwa mbali na kujiunga na kile tawala cha UDA, na kusisitiza kwamba mizizi yake katika siasa za humu nchini ni imara.
Kupitia kwa katibu wake mkuu ambaye pia ni mbunge wa Tongaren John Chikati, Ford Kenya imesema kwamba haina mpango wa kujiunga na UDA na badala yake kusisitiza kwamba kingali imara.
Chikati alikuwa ameandamana na viongozi wengine akiwemo naibu kinara wa chama hicho ambaye pia ni gavana wa Bungoma Ken Lusaka.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa