ECHOES OF WAR: MCHEZO WAMWEKA MALALA PABAYA
Huku tamasha za kitaifa za michezo ya kuigiza zikiendelea jijini Nakuru, aliyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala ameishutumu idara ya polisi kwa madai ya kutumiwa kumhangaisha kutokana na mchezo wa kuigiza aliouandika wa Echoes of War, ambao umeratibiwa kuwasilishwa na shule ya Butere Girls mapema leo kwenye tamasha hizo.
Hii ni baada ya polisi jana jioni kumzuia Malala kuingia katika shukle ya Kirobon High alikohitajika kuongoza matayarisho ya mwisho ya mchezo huo kabla ya kuwasilishwa.
Mchezo huo umeibua hisia mseto nchini, kutokana na maadhui yake yanayoonekana kukosoa ukandamizaji wa serikali dhidi ya haki za wakenya wachanga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































