#Local News

MASOMO VYUO VIKUU KUSAMBARATIKA

Huenda shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma nchini zikasambaratika tena kuanzia kesho iwapo serikali haitaingilia kati na kuepusha mgomo wa wahadhiri wa vyuo hivyo ambao wametangaza kuanza mgomo kuanzia leo usiku.

Wakizungumza na wanahabari, viongozi wa muungano wa wahadhiri UASU wakiongozwa na katibu mkuu Constantine Wasonga, wameilaumu serikali kwa madai ya kuwahadaa wakati wa kutia Saini mkataba wa maelewano mwezi mmoja uliopita kuhusu nyongeza ya mishahara yao.

Wameapa kwamba watagoma hadi matakwa yao yatakapotekelezwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MASOMO VYUO VIKUU KUSAMBARATIKA

WAUGUZI KISII KUSUSIA KAZI

MASOMO VYUO VIKUU KUSAMBARATIKA

JIEPUSHENI NA PROPAGANDA, RAIS RUTO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *