#Local News

JOPOKAZI LAUNDWA KUMPIGIA DEBE RAILA AFRIKA

Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi ameweka wazi mikakati ambayo serikali imeweka katika kumfanyia kampeni kinara wa Azimio Raila Odinga kwenye azma yake ya kuwania uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika AUC, akisema serikali imebuni jopokazi litakaloongoza kampeni hizo.

Katika kikao cha pamoja na wanahabari jijini Nairobi, Mudavadi amesema jopokazi hilo linahusisha viongozi kutoka serikalini na kikosi cha Raila, na kumtaja Raila kuwa kiongozi mwenye maono na kwamba ana uwezo wa kuibuka mshindi.

Kwa upande wake, Raila amesema alishtushwa na uamuzi wa serikali kuunga mkono azma yake, na kupongeza hatua ya serikali kubuni jopokazi hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *