#Football #Sports

NINA IMANI NA SALAH

Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher anaamini Mohamed Salah atataka kucheza kwa kiwango cha juu zaidi hadi atakapo timia umri karibia wa miaka 40, na analenga rekodi za Ligi Kuu na klabu licha ya kutokuwa na uhakika juu ya mustakabali wake.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri aliiweka timu yake katika mtihani wa maamuzi kuhusu mkataba wake baada ya kufunga na kutengeneza mabao mawili katika ushindi wa 3-0 wa Liverpool dhidi ya Manchester United Jumapili.

Salah ana umri wa miaka 32 lakini Carragher haamini kuwa hicho kitakuwa kikwazo kwa fowadi huyo na hivyo hafai kuwa hivyo pia kwa Liverpool.

Mnamo Julai 2022 Salah alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu, na kuripotiwa kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika historia ya klabu hiyo akipokea takriban Ksh.59 milioni kwa wiki.

Liverpool waliripotiwa kukataa pauni milioni 150 au Ksh 25 bn kutoka kwa Al-Ittihad ya Saudia kwa ajili ya Salah mwaka jana.

Mmisri huyo ameifungia Liverpool mabao 214 tangu ajiunge nayo mwaka 2017, na kumfanya awe nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

NINA IMANI NA SALAH

TUNAJIPANGA KWA MARATHON

NINA IMANI NA SALAH

STARLETS WAINGIA KAMBINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *