JUHUDI ZA KUREJESHA UTULIVU KISII-NAROK

Katika juhudi za kurejesha utulivu na kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii zinazosihi kwenye mpaka wa kaunti za Narok na Kisii, kamishna wa kaunti ya Narok Kipkoech Lotiatia amezitaka jamii hizo kusitisha uhasama na kukumbatia mazungumzo.
Akizungumza afisini mwake, kamishna huyo amesema polisi wanaendesha uchunguzi ili kurejesha ng’ombe walioibwa Pamoja na taarifa za mashamba kuchomwa moto.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa