#Basketball #Sports

HAIKUA RAHISI KWANGU

Kocha Msaidizi wa Equity Hawks, Samba Mjomba, amekiri kwamba haikuwa uamuzi rahisi kwake kutundika daluga za uchezaji na kujiunga na kazi ya ukocha.

Ligi ya Kikapu ya Kitaifa ya Wanawake ya 2023-2024 iliyomalizika hivi majuzi ilikuwa msimu wa kwanza kwa Mjomba kwenye benchi ya ufundi, baada ya kuacha kucheza mwishoni mwa msimu wa 2022-2023.

Mara moja alijiunga na benchi ya ufundi katika klabu hiyo ambayo alishinda mataji matatu ya ligi kuu kama mchezaji.

Mjomba alikiri kuwa amejifunza mbinu za ukocha kutoka kwa baadhi ya makocha bora nchini tangu alipojiunga na timu hiyo.

Nahodha huyo wa zamani aliongeza kuwa mengi yamebadilika katika sekta ya ukufunzi kwa miaka mingi, lakini akasema anaimarika vyema.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HAIKUA RAHISI KWANGU

WINCATE AJIUNGA NA SIMBA QUEENS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *