#Local News

GACHAGUA ATAKA DIG LANGAT ATIMULIWE

Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua ameshinikiza kufutwa kazi kwa naibu inspekta mkuu wa polisi wa kitengo cha polisi wa kawaida Eliud Langat kutokana na kifo cha mwanablogu Albert Ojwang’ Gachagua akisema Langat anafaa kuwajibishwa na wala si maafisa wa polisi waliosimamishwa kazi.

Kupitia taarifa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Gachagua amesema Langat anafaa kuwajibishwa kutokana na kukamatwa kwa mwanablogu huyo aliyetoa maoni yanayoonekana kumchafulia jina naibu huyo wa inspekta mkuu.

Kulingana na Gachagua, Langat anavitumia vituo vya polisi vya Kamukunji na Central kuwatesa wakenya bila ufahamu wa Inspekta mkuu wa Polisi Douglas Kanja, akisema ndiyo sababu ya kusafirishwa kwa Ojwang kutoka Homa Bay hadi kituo cha Central.

Imetayarishwa na Maureen Amakhobe

GACHAGUA ATAKA DIG LANGAT ATIMULIWE

UKAME WA MCCARTHY WAIBUA HOFU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *