GAVANA WA SIAYA JAMES ORENGO AMTAKA RAIS RUTO KUJIUZULU
Gavana wa Siaya James Orengo sasa anamtaka Rais William Ruto kujiuzulu akishikilia kuwa kuna hasira nyingi za umma dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza.
Kwa mujibu wa Orengo iwapo Rais Ruto angesikiliza hisia za watu nchini, angeweza kujiuzulu kwa sababu Wakenya wamechoshwa na utawala uliopo.
Kufuatia kutupiliwa mbali kwa Mswada wa Fedha wa 2024 ambao haukupendwa na watu Orengo amesema ni lazima Wakenya wajiandae kwa nyakati zijazo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































