#Local News

WACHIMBA MIGODI WA UGANDA WAATHIRI WAKENYA

Huenda hofu ya uchafuzi wa mazingira na tishio la maporomoko ya ardhi katika kaunti ya Busia ikafikia mwisho baada ya serikali kutangaza kufanya mashauriano na serikali ya Uganda kuhusu shughuli za uchimbaji migodi katika eneo la mpakani ambazo zimedaiwa kuharibu mazingira eneo hilo.

Akizungumza kwenye kaunti hiyo, Waziri wa masuala ya Jumuiya ya Afrika mashariki Askol Moe ameahidi kuzungumza na mwenzake wa Uganda kuhusu madai ya uvamizi wa raia wa Uganda wanaoendesha shughuli hizo.

Wakati uo huo, kamishna wa kaunti ya Busia Chaunga Mwachaunga na naibu gavana wa Arthur Odera, wamelalamikia ukosefu wa maji kutokana na shughuli hizo katika eneo la Amoni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WACHIMBA MIGODI WA UGANDA WAATHIRI WAKENYA

CHUO KIKUU CHA MOI CHAFUNGWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *