WABUNGE KENYA, UGANDA CHINI YA SHINIKIZO
Wabunge wa Kenya na Uganda wamejipata chini ya shinikizo, wakitakiwa kuziwajibisha serikali zao kuhusiana na taarifa za kuteswa kwa wanaharakati Boniface Mwangi na Agather Atuhaire wakiwa nchini Tanzania.
Mbali na kuwajibishwa kwa wahusika, mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yakiongozwa na chama cha wanasheria nchini LSK, yametaka serikali ya Tanzania kuwafidia wanaharakati hao.
Katika taarifa kwa wanahabari, mashirika hayo pia yameshinikiza mawaziri wa masuala ya kigeni wa Kenya na Tanzania kuweka wazi sababu za wawili hao kuteswa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































