UFARANSA, NAKURU KUSHIRIKIANA KUIMARISHA MAENDELEO

Balozi wa ufaransa humu nchini Arnaud Suquet serikali ya Ufaransa itashirikiana na serikali ya kaunti ya Nakuru kuimarisha sekta kama vile utalii, kilimo biashara, uwezeshaji wa wanawake na maendeleo ya teknologia ya habari na mawasiliano.
Akiwa kwenye ziara ya kaunti hiyo, Suquet ameitaja kaunti ya Nakuru kama kitovu cha kilimo katika kanda hiyo ya bonde la ufa na kupongeza mshikamano uliyopo katika kaunti hiyo yenye makabila mbalimbali.
Kwa upande wake, Naibu Gavana wa Nakuru David Kones amesema ziara hiyo inawiana na manifesto ya Gavana Susan Kihika pamoja na mpangilio wa maendeleo CIDP iliyozinduliwa hivi maajuzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa