ANSELMINO AINGIA CHELSEA

Chelsea imemsajili beki wa Boca Juniors Aaron Anselmino kwa ada ambayo haijawekwa wazi, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 atatolewa kwa mkopo katika timu hiyo ya Argentina kwa msimu wa 2024/25.
Anselmino ametia saini mkataba wa miaka saba Stamford Bridge, baada ya kucheza mechi 10 za wakubwa Boca, akianza na mechi yake ya kwanza ya kulipwa mnamo Juni 2023.
Anselmino, ambaye alifunga bao lake la kwanza katika maisha yake ya soka katika ushindi wa Copa Sudamericana dhidi ya Trinidense mwezi Aprili, ni mchezaji wa nane kusajiliwa na Chelsea katika dirisha hili la usajili.
Imetayarishwa na Nelson Andati