#Local News

KAGWE AAGIZA KUHARIBIWA KWA MBOLEA

Katika juhudi za kulinda ubora wa pembejeo na kuimarisha uzalishaji wa chakula, waziri wa kilimo na mifugo Mutahi Kagwe ameagiza kuharibiwa kwa magunia 27,518 na mbolea ambayo muda wake wa matumizi umepita ilhali ingali katika maghala ya nafaka kote nchini.

Kupitia taarifa mapema leo, Kagwe amesema zoezi la kuharibiwa kwa mbolea hiyo litasimamiwa na shirika la kutathmini ubora wa bidhaa KEBS iliyowasilishwa kati ya Disemba mwaka jana na Januari mwaka huu, akisema kampuni iliyowasilisha mbolea hiyo itagharamia hasara hiyo.

Ameitaka kuwasilisha mbolea yenye uwezo wa kudumu kwenye maghala kwa muda mrefu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KAGWE AAGIZA KUHARIBIWA KWA MBOLEA

MUTURI ATOA SABABU ZA KUKOSA VIKAO VYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *