KASI MAHAKAMANI YAPUNGUA, KOOME
Huenda utoaji haki mahakamani ukatatizika kutokana na ukosefu wa fedha, jaji mkuu Martha Koome akisema mahakama hazina uwezo wa kutekeleza majukumu yake kikamilifu baada ya mgao wa mwaka wa kifedha wa 2024-25 kupunguzwa.
Akizungumza katika mkutano na mabalozi na wawakilishi wa mataifa ya kigeni, Koome amesema kasi ya utoaji huduma imepungua kufuatia kupunguzwa kwa bajeti.
Idara hiyo imetengewa shilingi bilioni 21.6 kinyume na shilingi bilioni 44.9 iliyokuwa ikihitaji.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































