#Local News

RAIS RUTO ATAKIWA KUTULIZA JOTO NCHINI

Rais William Ruto ametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia katika kutuliza joto la kisiasa ambalo limepandishwa na mchakato wa kumbandua kutoka mamlakani aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua.

Katika kikao na wanahabari jijini Eldoret baada ya uteuzi wa Kithure Kindiki kujaza pengo lilioachwa na Gachagua, wakazi wa kaunti ya Uasin Gishu wamesema wana imani katika utendakazi wa uongozi mpya wa serikali, wakimsifia Kindiki kuwa mwenye uwezo wa kusaidia serikali kufanikisha ajenda yake ya maendeleo.

Wakati uo huo, wamelalamikia hali ngumu ya kiuchumi, wakimtaka rais kuchukua hatua za dharura kuangazia changamoto hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

RAIS RUTO ATAKIWA KUTULIZA JOTO NCHINI

NI KINDIKI, BUNGE LAIDHINISHA UTEUZI

RAIS RUTO ATAKIWA KUTULIZA JOTO NCHINI

GACHAGUA APATA AFUENI MAHAKAMANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *