HATUEGEMEI UPANDE WOWOTE
Rais Thomas Bach Amesisitiza Kwamba Kamati Ya Kimataifa Ya Olimpiki Haiegemei Upande Wowote Baada Ya Wito Wa Wapalestina Wa Kuitaka Israel Kuzuiwa Kushiriki Michezo Ya Paris Kutokana Na Vita Vya Gaza.
Wakati Timu Ya Israel Ikikaa Katika Kijiji Cha Wanariadha, IOC Ilichunguza Barua Kutoka Kwa Kamati Ya Olimpiki Ya Palestina Ikimtaka Bach Kuwapiga Marufuku Waisraeli, Ikitaja Vita Vya Ukanda Wa Gaza Kama Uvunjaji Wa Makubaliano Ya Olimpiki.
Ilisema “Takriban Wanariadha 400 Wa Kipalestina Wameuawa Na Uharibifu Wa Vifaa Vya Michezo Unazidisha Masaibu Ya Wanariadha Ambao Tayari Wako Chini Ya Vikwazo Vikali”.
Wito Wa Wapalestina Unaangazia Jinsi Idadi Ya Vifo Inayoongezeka Na Kuongezeka Kwa Mzozo Wa Kibinadamu Huko Gaza Kunavyoathiri Michezo Ya Paris.
Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Ufaransa Tayari Amelazimika Kuingilia Kati Kusisitiza Kwamba Wanariadha Wa Israel Wanakaribishwa Baada Ya Mwanasiasa Wa Siasa Kali Za Mrengo Wa Kushoto Wa Ufaransa Kutaka Wazuiliwe Kutokana Na Mashambulizi Ya Gaza.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































