MTOTO WA MIAKA MIWILI APATIKANA AKIWA AMEKUFA ENEO LA GATHARAINI KASARANI

Polisi wanachunguza kifo cha mtoto wa miaka 2 ambaye mwili wake umepatikana kando ya mto Gatharaini eneo la Kasarani jijini Nairobi.
Inaarifiwa kuwa mwili huo umepatikana na mkaazi mmoja wa eneo hilo alipokuwa akisafisha mtaro wa maji.
Mwili wa mtoto huyo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya city ukisubiri kufanyiwa upasuaji.
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































