VIONGOZI WATUMAI ODINGA ATASHINDA

Viongozi wakuu serikalini wamesema wana matumaini kwamba kiongozi wa Azimio Raila Odinga atafanikisha utatuzi wa changamoto nyingi zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika bara la Afrika, iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa tum e ya umoja wa Afrika AUC.
Wakiongozwa na Waziri wa mazingira Aden Duale, John Mbadi wa fedha na Alice Wahome wa ardhi, wamesema serikali ya Kenya Kwanza itaendelea kumuunga mkono Odinga katika azma yake ya kuwania wadhifa huo.
Wakati uo huo, Odinga amesikitikia hatua ya bara hili kusalia maskini licha ya wingi wa raslimali za kiasili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa