SENETI YAMHOJI WAZIRI MVURYA

Waziri wa madini na raslimali za majini Salim Mvurya amehojiwa na kamati ya seneti kuhusu raslimali za madini katika kaunti mbali mbali.
Waziri huyo ametakiwa kutoa maelezo kamili kuhusu jinsi wakazi watakavyonufaika na asilimia 10 ya mapato yanayotokana na madini
Kwa upande wake, kiranja wa wengi katika bunge hilo Boni Khalwale, amelalamika kuhusu mahangaiko ya wachimba migodi nchini licha ya idara hiyo kuchangia pakubwa katika pato la taifa.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa