MHASIBU WA MAGEREZA GEREZANI
Aliyekuwa mhasibu wa serikali katika idara ya huduma za magereza Humphrey Abok ameshtakiwa kwa ulaghai wa mali ya umma yenye thamani ya shilingi milioni 302.
Abok na washukiwa wenza wanatuhumiwa kuilaghai serikali kwa kupokea malipo ya bidhaa ambazo kamwe hazikutolewa.
Abok amekanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni saba au dhamana mbadala ya pesa taslimu shilingi milioni nne.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe tatu mwezi septemba mwaka huu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































