#Football #Sports

AL ALHY WAIADHIBU GOR MAHIA MABAO 3-0

Miamba wa soka kule misri, Al Ahly, waliwacharaza vigogo wa kandanda humu nchini Gor Mahia mabao 3-0 katika uga wa Nyayo jumapili jioni.

Al Ahly sasa imefufua matumaini yao ya kutinga awamu ya muondoano kwenye dimba la klabu bingwa barani africa. Wao ndio mabingwa watetezi, na wamenyakua taji hilo mara 12.

Ni mechi ambayo wana gor mahia walianza kwa kunoa makali yao, na kuonyesha kiu na ari ya kufunga mabao ila Al Ahly waliwazidi maarifa.

Hii sasa inawaacha Gor Mahia na kibarua kikubwa cha kushinda mechi ya raundi ya pili kule Cairo- Misri wikendi ijayo.

Ndani ya robo saa, wageni walikuwa kifua mbele kwa mabao 2-0, na hatimaye kufunga bao la mwisho.

Gor mahia walipata jaribio lao la kwanza la kulenga lango, maarufu on target baada ya dakika 23.

Imetayarishwa na Kennedy Osoro

AL ALHY WAIADHIBU GOR MAHIA MABAO 3-0

CHIRCHIR: HAKUNA ARDHI HURU KWA ADANI

AL ALHY WAIADHIBU GOR MAHIA MABAO 3-0

WAZIRI WA MICHEZO MURKOMEN NA RAIS WA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *