CHIFU AKAMATWA GARISSA KWA KUCHUKUA HONGO

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemkamata chifu katika Kaunti ya Garissa kwa madai ya kuwaibia wakimbizi wanaotafuta huduma katika afisi yake.
Katika taarifa EACC jana Jumanne ilisema kwamba Abdirahman Shafe Yussuf, Chifu wa eneo la Bulla Mzuri, amekuwa akidai hongo kutoka kwa wakimbizi katika mchakato unaoendelea wa kufuta alama za vidole kutoka kwa mfumo wa UNHCR.
Imetayarishwa na Janice Marete.