KENGEN INAWAHAKIKISHIA WATUMIAJI NISHATI YA MAJI YA BEI NAFUU
Wateja wataendelea kufurahia manufaa ya nishati ya bei nafuu ya umeme wa maji, haya ni kwa mujibu wa kampuni ya kutoa huduma hizo KenGen huku ikiendeleza mpango wake wa usimamizi wa maji ambao umehakikisha uzalishaji wa umeme unaotokana na maji hata baada ya mvua kupungua.
Kampuni hiyo pia imewahakikishia wanajamii wanaoishi chini ya Mabwawa ya Seven Forks kwamba mtiririko wa maji katika Mto Tana utaendelea kuwa shwari, hata kama nchi inakabiliwa na kupungua kwa mvua.
Katika taarifa usimamizi wa kimkakati wa mabwawa yake makubwa katika eneo la Mashariki una jukumu muhimu katika kudhibiti viwango vya maji, kuhakikisha mtiririko thabiti wa Mto Tana.
Usimamizi umebainisha kuwa Bila afua hizi, mto unaweza kukabiliwa na upungufu mkubwa unaotokana na kupungua kwa mvua, kuathiri jamii, kilimo, na wanyamapori wanaotegemea maji yake.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































