MACHOGU APUUZA KAULI ZA WALIMU WAKUU
Waziri wa elimu Ezekiel Machogu, ameendelea kupuzilia mbali kauli za baadhi ya walimu wakuu wa shule za umma kwamba watafunga shule mapema kutokana na mgao wa elimu.
Akizungumza jijini Nairobi, Machogu amesema mgao huo utatolewa kwa wakati ufaao.
Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha wazazi Cyrus Obuhatsa, amesema sughuli za masomo katika shule za umma zinatatizika kutokana na kucheleweshwa kwa mgao huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































