WAJIBIKENI AMA MUENDE, RUTO AWAAMBIA MAAFISA

Wakenya wanatarajia huduma bora kutoka kwa serikali kuanzia sasa baada ya Rais William Ruto kuwaagiza mawaziri na makatibu wao watekeleze wajibu wao ipasavyo la sivyo wafutwe kazi.
Akiwahutubia katika hafla ya kutia saini kandarasi ya utendakazi katika Ikulu ya Nairobi, Rais ametetea utendakazi wa serikali yake na kuahidi mageuzi Zaidi katika sekta kadhaa ikiwemo afya, nyumba, kilimo na elimu.
Aidha, Rais ambaye amewapa kandarasi watumishi wa umma kwa mara ya pili sasa, amewalaumu baadhi yao kwa kuzembea kazini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa