MAFURIKO YAZUA HOFU NAKURU

Hofu ingali imetanda katika eneo la Kaptembwo kaunti ya Nakuru baada ya mtu mmoja kufariki na makumi ya familia kuachwa bila makao kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa.
Sammy Tarus amepoteza uhai baada ya kusombwa na mafuriko kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea Eldoret, vidimbwi sasa vikiwa vimeanza kuchimbika kando kando mwa barabara hiyo na kuzua hofu ya maporomoko.
Mwili wake umeopolewa mapema leo na kupelekwa katika hifadhi ya hospitali ya Nakuru.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa