MSWADA WA BAJETI 2024-2025 UMEZIDI KUIBUA TUMBO JOTO

Mswada wa bajeti wa mwaka wa 2024-2025 umeibua hisia kinzani miongoni mwa wakenya kuhusu mapendekezo yaliyomo kuhusu kuongezwa kwa kodi.
Rais William Ruto ametetea mswada huo akisema kwamba wanalenga kuongeza mapato ya taifa na hatimaye kuimarisha uchumi wa taifa.
Kwa mujibu wa rais Ruto kuongeza kodi kutasaidia kupunguza kutegemea mikopo kutoka mashirika mbali mbali yakiwemo kimataifa ili kujiendeleza.
Viongozi wa azimio wamewarai wabunge wake kutounga mkono mswada huo wakiutaja kuwa wa kuwakandamiza wakenya.
Wakiongozwa na kiongozi wa chama cha wiper Kalonzo Musyoka ,viongozi hao wametishia kurejelea maandamano ili kupinga mswada huo.
Imetayarishwa na: Janice Marete