DATA YA BEI NAFUU HUVUTIA MTANDAO WA SETILAITI UNAPOANZA KUIMARIKA

Mwaka mmoja baada ya kuanzishwa kwa mtandao wa satelaiti wa kiwango cha kibiashara na Elon Musk’s Starlink barani Afrika, maendeleo makubwa yanaanza kurekebisha sura ya mtandao ya bara hili.
Mtandao wa bei nafuu na wa haraka unazidi kupatikana kadiri utolewaji wa miundombinu ya setilaiti unavyoongezeka na ushindani kati ya watoa huduma unavyoongezeka.
Mnamo Mei, Liquid Intelligent Technologies, mhusika mkubwa wa utoaji wa huduma za Intaneti iliyo na uwepo katika nchi 14 barani Afrika, ilishirikiana na OneWeb kupanua ufikiaji wa mtandao hadi maeneo ya mbali na kuahidi kutoa muunganisho bora, kwa kutumia obiti ya chini ya Dunia na satelaiti za jadi.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi