NI TALAKA SASA- WAMALWA

Kiongozi wa chama cha DAP -K Eugene Wamalwa amesema kuwa muungano wa Azimio umefikia hatua ya kuvunjiliwa mbali, akisema ni usaliti kwa muungano huo kufanya kazi na serikali.
Kwa mujibu wa Wamalwa, hatua ya chama kimoja kukubali kufanya kazi na serikali ni kinyume na kanuni za muungano huo, na hivyo ni vigumu kwa vyama tanzu kusalia katika Azimio.
Hata hivyo, Waziri huyo wa zamani amesema mazungumzo miongoni mwa vyama tanzu ili kutatua suitofahamu iliyopo, ingawa tayari chama tanzu cha Narc Kenya kimetangaza kuondoka
Imetayrishwa na Antony Nyongesa