UKAGUZI WA DETA MARIGO-INN

Zoezi la kukusanya na kukagua deta za wakazi wa mtaa wa Maringo-inn eneo la Nairobi South linatarajiwa kuanza wikendi hii, zoezi likijiri wakati ambapo wakazi wametakiwa kuondoka mtaani humo kwa muda ili kuruhusu ujenzi wa makazi ya bei nafuu.
Afisa katika idara ya ujenzi katika serikali kuu Gabriel Muli anayeongoeza zoezi hilo hata hivyo amewahakikishia wakazi kwamba serikali itawafidia ipasavyo.
Naye mwakilishi wa wadi ya Nairobi South Waithera Chege amewataka wakazi kukumbatia mradi huo anaosema utawafaa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa