‘FUATA SHERIA UKIUZA MIRAA AU MUGUKA’ GAVANA ABDULLSWAMAD SHERRIF NASSIR ASEMA

Gavana wa Mombasa Abdullswamad Sherrif Nassir amekataa kata kata kubadilisha uamuzi wake wa kuweka masharti mapya katika uuzaji wa miraa na muguka katika kaunti hiyo.
Masharti hayo mapya serikali ya Mombasa imeweka ada ya shilingi elfu 8 kwa kila gari inayosafirisha miraa katika kaunti hiyo.
Kadhalika ametoa notisi ya siku 7 kwa maduka ya kawaida ambayo pia yanauza miraa na muguka akisema bidhaa hizo zinafaa kuuzwa katika maduka maalum kando na yale yanayouza bidhaa nyingine.
Vile vile amepiga marufuku utumiaji wa miraa katika uchukuzi wa umma wakati wa kazi na kupiga marufuku magari hayo ya uchukuzi wa umma kusafirisha bidhaa hiyo na watakaopatikana watatozwa faini ya elfu 8.
Nassir amesema masharti hayo yatatekelezwa licha ya gavana wa Enbu Cecil Mbarire na seneta wa meru Kathuri Murungi kumtembelea na kumshawishi kulegeza baadhi ya masharti.
Imetayarishwa na: Janice Marete