WAKENYA WATAKIWA KUWASILISHA MAOMBI YA KAZI ILI KUPATA AJIRA UJERUMANI
Wakenya ambao wana taaluma na ambao wangependa kufanya kazi nje ya nchi wametakiwa kutuma maombi yao ya kazi.
Katibu katika wizara ya maswala ya kigeni Roseline Njogu ameutetea mpango wa serikali wa kuwatuma wakenya kufanya kazi ugaibuni.
Akitoa maelezo zaidi kuhusu mkataba wa kenya na ujerumani Njogu amesema kuwa wakenya wataonufaika kwa kupata ajira ujerumani ni wale wenye taaluma na kwamba watahitajika kutuma maombi kwanza.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































