WAZIRI WA ELIMU MACHOGU AAGIZA HELB KUFUNGUA TOVUTI YA UFADHILI KWA WANAFUNZI KUTUMA MAOMBI

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu ameamuru Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) na Hazina ya Vyuo Vikuu (UF) kufungua tovuti ya ufadhili kuanzia Juni 15, ili kuruhusu wanafunzi wanaohitimu kutuma maombi yao
Amri hiyo inajiri baada ya Rais William Ruto mwezi Mei kutambulisha muundo mpya wa ufadhili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na na vyuo vya kiufundi TVET nchini Kenya, kufuatia mashauriano ya kitaifa yaliyofanywa na Chama cha Rais kuhusu Marekebisho ya Elimu.
Imetayarishwa na Janice Marete