JIEPUSHENI NA PROPAGANDA, RAIS RUTO

Propaganda na taarifa za kupotosha zimerejesha nyuma juhudi za serikali kutekeleza ahadi zake kwa wakenya, Rais William Ruto akiwataka wakenya kujiepusha na habari hizo na badala yake kushirikiana na serikali katika kuboresha maisha yao.
Akizungumza wakati wa hafla ya kufuzu kwa maafisa wa idara ya misitu, rais Ruto ameimiminia sifa idara hiyo katika kuimarisha juhudi za kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Naye Waziri wa mazingira Aden Duale aliyekuwa ameandamana na Rais, ameahidi juhudi zaidi za kuboresha mazingira nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa