NEWCASTLE YASHINDA KOMBE LA LIGI KWA KUICHAPA LIVERPOOL 2-1

Newcastle ilishinda Kombe la Ligi baada ya kuilaza Liverpool 2-1, huku Dan Burn na Alexander Isak wakifunga mabao muhimu.
Huu ni ushindi wao wa kwanza mkubwa tangu 1969 na taji lao la kwanza la ndani tangu 1955 ushindi ambao unajiri baada ya kupoteza fainali ya 2023 dhidi ya Manchester United.
Kwa Liverpool, kichapo hiki ni pigo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini bado wanaongoza Ligi Kuu kwa alama 12.
Imetayarishwa na Janice Marete