“HATUWATAMBUI!” WAANDAMANJI BUNGOMA
Vijana kutoka maeneo bunge ya webuye magharibi na webuye mashariki kaunti ya Bungoma wameandamana mjini Webuye huku wakiwakosoa wabunge wao ambao ni Dan Wanyama na Martin Wanyonyi kwa kupiga kura ya ndio kuhusu mswada wenye utata juma lililopita.
Wakati wa maandamano hayo, kijana mmoja aliyejitokeza kupinga maandamano hayo amejeruhiwa vibaya na waandamanaji.
Aidha, vijana hao wamelalamikia hali ngumu ya Maisha, wakiapa kuendelea na maandamano hayo hadi kilio chao kitakaposikilizwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa.
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































