KIKOSI CHA PILI CHATUA PARIS

Kundi la kwanza la timu ya Kenya ya Olimpiki ya walemavu limetua jijini Paris tayari kwa mashindano hayo yaliyo ratibiwa kufanyika Agosti 28 hadi Septemba 8.
Mkurugenzi wa Michezo Jaxon Indakwa alisema kikosi hicho kitaelekea moja kwa moja kwenye kambi ya Timu ya Kenya ya Olimpiki ya Walemavu mjini Compiègne.
Mary Njoroge, ambaye atashiriki katika mbio za mita 1500 kitengo cha T11, ana nia ya kuibuka na medali mwaka huu baada ya kushindwa kufika fainali huko Tokyo miaka mitatu iliyopita.
Kenya itawakilishwa na wanariadha 14 na waongozaji saba katika vitengo vitano kwenye Michezo ya Paris.
Imetayarishwa na Nelson Andati