HATUPO KWENYE MASHINDANO
Kocha mkuu wa Kisumu RFC Oscar Okaron amefichua kuwa timu yake haitashiriki mkondo wa tano wa msururu wa Kitaifa wa raga ya wachezaji saba nchini, Driftwood 7s, Mombasa wikendi hii, kutokana na majeraha kadhaa katika kikosi chao chembamba.
Kisumu bado haijaandikisha ushind wowote katika shindnao hili licha ya kuwa mwenyeji wa mkondo wa tatu, Dala 7s, na Okaron anakiri kuwa wanatatizika kuijenga upya timu hiyo kufuatia kuondoka kwa wachezaji wao nyota.
karon anasema lengo lao ni kuandaa timu kwa ajili ya ligi kuu nchini ambayo itaanza baada ya muda wa mwezi mmoja.
Okaron pia alisikitikia kuendelea kwa uwindaji wa wachezaji kutoka timu za kijamii, jambo ambalo linawafanya washindwe kufurukuta wanapokabiliana na timu zilizoimarika kama vile Kabras Sugar, KCB na Kenya Harlequin.
Driftwood 7s itashuhudia Mombasa RFC, ambayo haijacheza katika msururu wa mwaka huu, ikishiriki Ligi ya Divisheni ya Kwanza kwa heshima ya kuwa mwenyeji huku mashindano hayo yakikaribia mwisho.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































