KAWI GHALI YAATHIRI AFYA, KILIMO
Kongamano la mawaziri wa kawi kutoka kaunti zote 47 linaendelea kwa siku yake ya pili katika kaunti ya Makueni huku gavana wa kaunti hiyo Mutula Kilonzo Junior akisema kwamba gharama ya kawi ni ya juu, na kwamba imeathiri utendakazi wa serikali hizo.
Kongamano hilo linalenga kujadili mwafaka kuhusu kawi safi nay a bei nafuu ili kupunguza gharama ya utengenezaji wa bidhaa na uendeshaji wa shughuli za kaunti.
Kulingana na gavana huyo, gharama ya kawi imeathiri hasa sekta ya afya na ile ya kilimo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































