MWANAMUME AKAMATWA KWA UHARIBIFU WA MAGARI KIAMBU
Mwanaumme mmoja anayedaiwa kuvunja nyumba eneo la kiamumbi kaunti ya Kiambu na kuharibu magari kisha kuiba vipuri vyake amekamatwa.
Kwa mujibu wa polisi mshukiwa kwa jina Francis Ndichu Kimani maarufu Ndich amepatikana akipanda ukuta wa nyumba moja eneo la Santiago hatua iliyopelekea kukamatwa kwake.
Mshukiwa anatarajiwa kufikisha mahakamani.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































